Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameiomba Taasisi ya Africa Academy for Public Health kushirikiana na Serikali kufanya tafiti zenye tija kwenye magonjwa kama TB na Ukimwi ili kupunguza changamoto ya magonjwa hayo nchini.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2018 hadi 2020 wa taasisi Africa Academy for Public Health Jijini Dar Es Salaam. Mkakati huo ua lengo la kukuza tafiti za mfumo wa afya, ubunifu na matumizi ya takwimu katika kuboresha ustawi wa watu.
Dhima ya Taasisi ya ya Africa Academy for Public Health ni pamoja na kushirikiana na Serikali, wadau wa afya katika tafiti mbali mbali za afya hususani zinazohusu afya ya mama na watoto masuala ya lishe, magonjwa yasiyo ya kuambukiza na yale ya kuambukiza.
Picha na mtandao.