Wadau wa Kahawa mkoani Kilimanjaro wamepongeza hatua ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuvunja mfuko wa maendeleo ya zao la Kahawa (CDTF) wakieleza kuwa mfuko huo ulikuwa ni mzigo kwa wakulima kutokana na tozo mbalimbali.

Meneja mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) chenye vyama wanachama 92 wanaojishughulisha na Kilimo cha zao la Kahawa, Honest Temba amezungumza na Star TV na kupongeza hatua hiyo.

Gabriel Ulomi ni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi Lyamungo na meneja miradi wa kikundi cha Wakulima wa zao la Kahawa kijulikanacho kama G32 hapa anaeleza changamoto nyingine ambazo serikali inapaswa kuziangalia. .

Mapema hivi karibun. Naibu Waziri wa Kilimo, Marry Mwanjelwa ametembelea Makao makuu ya Bodi ya Kahawa (TCB) yaliyopo mkoani Kilimanjaro na kuzungumza na watendaji wa bodi hiyo kuhusu kumuinua mkulima wa zao la Kahawa.

Mfuko wa Maendeleo wa zao la Kahawa (CDTF) umevunjwa baada ya kubainika uundwaji wake haukufuata sheribali uliundwa na wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na bodi ya kahawa Tanzania (TCB).

Picha na mtandao.

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.