Serikali imewatoa wasiwasi wakulima wa Pamba mkoani Morogoro juu ya upatikanaji wa soko pamoja na pembejeo ambapo mnunuzi atakayenunua Pamba yote itakayozalishwa amepatikana.

Akizungumza na wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Makuyu wilayani Mvomero mkoani hapa, mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr.Kebwe Stephen, amesema historia inaonyesha mkoa wa Morogoro ndio mwasisi wa kilimo cha zao la Pamba, na lilikuwa tegemeo kubwa la kiuchumi kwa wakulima na Serikali ya mkoa.

Dr Kebwe amesema serikali inatambua changamoto zilizopelekea baadhi ya wakulima kuamua kuachana na kilimo cha zao hilo, hususani kukosekana kwa soko la uhakika, jambo ambalo limeshapatiwa ufumbuzi.

Marco Mtunga ni mkurugenzi wa bodi ya Pamba nchini ,amesema wakulima wa zao la pamba wana fursa kubwa kupiga hatua kiuchumi ikilinganishwa na mazao mengine ya biashara, hivyo kuwataka kuwatumia wataalamu wa kilimo katika maeneo yao, na kufanya kilimo chenye tija.

Na hapa baadhi ya wakulima wa zao la pamba wilayani Mvomero,wakabainisha changamoto mbalimbali zilizokwamisha kilimo cha zao hilo.

Pamba ni kati ya mazao matano ya biashara yaliyopewa kipaumbele na serikali ya wamu ya tano kutaka kufanikisha adhma ya serikali ya viwanda na nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025 ambapo makisio kwa wilaya ya Mvomero pekee ni kufikia wastani wa tani 293 za mavumo kwa msimu wa kilimo 2017/2018 huku wakulima zaidi ya 290 wamehamasika kujikita katika kilimo hicho.

Picha na mtandao.

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.