Star Tv

Wizara ya mambo ya ndani kupitia idara ya uhamiaji mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi (JWTZ) imewakamata wahamiaji 67 wasiofata sheria na wenye uraia wa nchini Ethiopia.

Raia hao ambao walikua walielekea nchini Msumbiji kwa njia ya bahari waliongozwa na mtanzania kutoka visiwa vya Pemba ajulikanae kwa jina la Bakari Ally.

Wahamiaji hao walikuwa wakitoka Mombasa nchini Kenya wakielekea nchini Afrika Kusini na kati yao ni mmoja tu ndiye anayejua lugha ya kiingereza.

Akiongea na waandishi wa habari Afisa uhamiaji wa mkoa wa Mtwara James Mwanjotile amesema watu hao 67 kati yao ni 14 tu wenye vibali vya kusafiria yaani passport lakini hawakupita katika vituo vya uhamiaji kwa ajili ya kufuata taratibu za kusafiri.

Aidha wahamiaji wengine 7 wamekamatwa wilayani Tandahima na kufanya jumla ya wahamiaji kufikia 74 ambao tayariwamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini bila kufuata taratibu.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.