Star Tv

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Camilius Wambura ameunda tume huru kuchunguza tukio la mauaji ya watu wawili waliouawa baada ya askari kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto katika vurugu zilitokea Kijiji cha Ikwambi Kata Mofu Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

IGP. amesema tume hiyo itakuwa chini ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi ambapo itachunguza chanzo cha tukio hilo na kutambua endapo kulikuwa na sababu za kutumia risasi za moto katika kukabili vurugu zilizokuwepo zilizohusisha wafugaji ambao walikamatwa na kuwafungia viongozi kadhaa wa Kijiji hicho.

Tukio hilo lilitokea jana Oktoba 23, 2022 na kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amesema chanzo ni wakulima ambao ni wakazi wa kijiji hicho kuwafungia ndani ya ofisi ya Kijiji wenyeviti wa vitongoji, vijiji pamoja na Wafugaji kwa lengo la kutaka kuwachoma Moto wakiwatuhumu kushindwa kuwasaidia pindi wafugaji wanapoingiza mifugo katika mashamba yao.

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni Diwani wa kata hiyo Greyson Mgonela, ambaye baada ya kufanya mazungumzo naye kwa njia ya simu amesema wakati vurugu zinatokea wananchi walikuwa wakitumia silaha za jadi, Mawe, Mikuki na Marungu kuwapiga Askari, huku Askari nao wakitumia Mabomu ya Machozi na Kisha Risasi za Moto.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.