Star Tv

Rais Samia Suluhu Hassan amekemea tabia ya baadhi ya viongozi kutochukua hatua dhidi ya ubadhirifu na miradi isiyoendana na thamani ya fedha katika maeneo yao ya kiutendaji hadi pale mbio za Mwenge zinapokuja kubaini kasoro zilizopo katika miradi hiyo.

Rais Samia ametoa agizo hilo wakati akilihutubia Taifa katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ,wiki ya vijana pamoja na kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa  zilizofanyika katika uwanja wa Kaitaba, Ambapo amewataka watanzania kuendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuendelea kupiga vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

''Nami nitumie fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuendeleza kuwaenzi wazee wetu hawa, kumuenzi baba wa taifa, kwa kupinga vitendo vya ufisadi, rushwa, chuki, dharau na kuuenzi umoja na mshikamano" - Rais Samia.

Aidha amezitaka mamlaka za kupambana na rushwa za TAKUKURU na ZAECA kufanya uchunguzi wa kina katika miradi iliyokataliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru.

Awali kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2022 Sahili Geraruma licha ya kuipongeza sekta ya maji kwa kufanya vizuri ameelezea baadhi ya kasoro zilizobainika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ununuaji vifaa kwa bei ndogo huku fedha nyingine wakizifuja.

Waziri wa Kazi, vijana, Ajira na wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema mbio za Mwenge zimekuwa na matokeo chanya huku Waziri wan chi ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Hamza Juma akiwataka watanzania kuendelea kuwaunga mkono viongozi wa serikali kwa juhudi zao za kuwaletea maendeleo watanzania.

Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu 2022 umetembea kilomeita 39,273 katika halmshauri 195 na kukagua miradi 1293 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 650.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.