Pembejeo feki za kilimo zimetajwa kuharibu mpango wa serikali wa uanzishwaji wa Viwanda nchini, huku zikidaiwa kudumaza hali ya uchumi wa wakulima kwa kushindwa kupata mavuno yale waliyokusudia na hivyo kujikuta wakiendesha kilimo kisicho na tija.
Ni msimu wa kilimo ambapo wakulima katika mikoa mbalimbali nchini wapo mashambani kutimiza wajibu wao, huku changamoto ya uuzaji wa pembejeo feki inayofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa kusambaza na kuuza mbegu zisizofaa inadaiwa kukinzana na matamanio ya serikali ya awamu ya tano inayohimiza viwanda ambavyo malighafi zake nyingi zinategemea mavuno yatokanayo na kilimo
Changamoto nyingine zilizotajwa na wakulima kuwa ni kuchelewa kwa pembejeo za ruzuku.
Umoja wa wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo mkoa wa Njombe, kupitia katibu wake Waziri Kindamba amesema suala la uuzaji wa pembejeo feki wanalikabili ipasavyo na kuwa wao kama wafanyabiashara changamoto kuu ni namna ya kuwafikia wakulima wa pembezoni na bei elekezi.
Picha na mtandao.