Serikali imeshauriwa kutumia umeme wa nguvu za jua kwenye taasisi zake hasa hospitali na shule ili kuongeza ufanisi wa Huduma za afya na ufaulu kwenye sekta ya elimu nchini.
Mkurugenzi wa meza ya pamoja ya maafisa watendaji wakuu wa taasisi nchini CEO Round-table ametoa ushauri huo wakati akizindua mradi wa umeme wa nguvu za jua wa kampuni ya Mobisol.
Umeme wa nguvu za jua ni mojawapo ya nishati zinazotumiwa na wakazi nchini ambapo inatajwa kuwa endapo taasisi za Serikali kama hospital na vituo vya afya zitautumia umeme huo vitafanya kazi kwa ufanisi kutokana na kuwa na uhakika wa upatikanaji wake.
Picha na mtandao.