Serikali imetakiwa kuangalia upya mfumo wa stakabadhi ghalani kutokana na wanunuzi kuchelewa kufanya malipo tangu siku ya mnada.
Siku nne baada ya mnada wanatakiwa kulipa na kutoa mzigo wa Korosho ghalani ili kuingiza mzigo mwingine.
Wakulima na wajumbe wa bodi ya korosho ya Amcos ya kata ya kikongo kijiji cha kikongo wamemkatalia mnunuzi wa korosho aliyenunua siku ya mnada zikiwa daraja A katika kuchelewa kulipa na kutoa korosho huku akitaka kupima ubora wa korosho kwa mara tatu, ndipo wakulima wakapaza sauti zao kwa serikali.
Chama cha msingi cha Amcos kikongo tayari wameshaingiziwa fedha zao kupitia ankaunti ya Corecu huku wanachama wakiwa wameanza kusaini ili kupatiwa fedha zao.
Picha na mtandao