Star Tv

Tanzania hupoteza miti zaidi ya milioni 38 kila mwaka kutokana na matumizi mbalimbali ya kibinadamu hatua inayoelezwa kuwa huenda ikasababisha nchi kuingia katika jangwa miaka 15 ijayo iwapo hatua za dhati hazitochukuliwa kupambana na tatizo hilo.

Dr. Felisian Kilahama amezungumza na viongozi na watendaji wa kata ya Nyegina iliyopo wilayani Musoma katika semina na kuzitaka taasisi zinazosimamia masuala ya mazingira kupambanua kwa nguvu zote na tatizo hilo ili nchi isiingie katika jangwa.

Akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Musoma,Katibu tawala wa wilaya hiyo,Jackson Manko,amepiga marufuku ukataji miti ovyo na kuwataka watendaji kusimamia upandaji wa miti million tatu .

Kwa upande wao wadau wa mazingira katika wilaya hii wameshukuru kwa kujengewa uwezo ili kujua wajibu wao na kusema kuwa watahakikisha wanasimamia upandaji miti katika maeneo yao.

Shirika la umoja wa maendeleo Bukwaya,Umabu,linafanya mafunzo katika vijiji zaidi ya 22 vilivyopo katika kata tano za Nyegina, Nyakatende, Etaro, Efurifu na Bisumwa vilivyopo wilayani Musoma mkoani Mara ili kuwajengea uwezo viongozi na watendaji kusimamia uhifadhi wa mazingira.

Picha na mtandao

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.