Star Tv

Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa kushirikiana na wataalam kutoka mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili wametoa mafunzo kwa takriban Waandishi wa Habari 25 kutoka vyombo mbalimbali nchini ambavyo ni TV, Redio, pamoja na Magazeti.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku Tatu jijjini Dar es Salaam kwa baadhi ya waandishi huku wengine wakifuatilia kwa njia ya mtandao yalikuwa ni kwa ajili ya kuwanoa waandishi kuweza kuwa mstari wa mbele katika uhifadhi kwa lengo la kuuendeleza urithi wa maliasili pamoja na malikale.

Hatua hii imefikiwa na shirika hilo likamini kuwa mafunzo hayo yatawasaidia waandishi kuandika habari kwa wigo wa kuangalia na kuzingatia kanuni na sheria zinazolinda na kuzuia uharibifu wa mazingira pamoja uwindaji haramu wa wanyamapori.

Aidha, awali akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa JET Dkt. Ellen Outara amewataka Waandishi wa Habari kutumia mafunzo hayo vema ikiwa ni pamoja na kuandika habari zitakazoigusa jamii katika kuendelea kuhifadhi maliasili kwa vizazi vijavyo.

Mtaalam kutoka mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili Bwana Joseph Olila aliwasihi waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele na kupaza sauti kwa jamii kwa kuandika habari zenye kuifanya jamii itambue mipaka yao na wanyamapori katika “shughuli zao za kibinadam” kutozidi mipaka kwa manufaa ya kuhakikisha haziathiri shoroba za wanyamapori pamoja na sehemu zao za malisho.

“Waandishi nyinyi mnayo nafasi kupaza sauti kwa umma katika hili suala la ushiriki wa kusimamia mchakato wa kupanga ardhi kwa manufaa ya wanyama ili kuongeza kasi ya uelewa kwamba shughuli za kibinadamu hazipaswi kuzidi mipaka, na matumizi ya ardhi yanapaswa kuzingatia pande zote”-Alisema Bw. Olila.

Kwa upande wake Afisa mtandao wa ufuatiliaji biashara ya Wanyamapori Allen Mgaza wakati wa wasilisho lake la mafunzo kwa waandishi aliwasisitiza kuhakikisha wanaibua biashara haramu za viumbe bahari na wanyama ambavyo vimepigwa marufuku biashara yake lakini baadhi ya wananchi huifanya kwa kujua ama laah kutokujua.

“Kuna viumbe bahari baadhi ni marufuku kuvifanyia biashara lakini vinauzwa huko mtaani,…..Pia kuna watu wanauza mafuta ya simba kama dawa, kucha za simba, ngozi za chui n.k na sio rahisi kuwagundua, lakini nyinyi waandishi hiyo ni kama 'tip' unaweza kuifuatilia na kuandika habari itayoelimisha jamii kwa ujumla”-Alisema mgaza.

Mradi huo wa kutoa mafunzo unaofanywa na JET ukiwa umedhaminiwa na USAID Tuhifadhi Maliasili ambao utafanyika kwa miaka mitano unatazamiwa kuleta mwitikio chanya wa kumaliza suala la ujangili, uharibifu wa shoroba za wanyamapori kwa kuendeleza mazingira, uhifadhi na utalii hapa nchini.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.