Star Tv

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge kufuatilia kwa karibu ujenzi wa eneo la maegesho ya magari katika kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo ambalo ujenzi wake umekuwa ukisuasua.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tano mkoani Kagera baada ya kubaini kuchelewa kwa ujenzi wa eneo la maegesho unaoendelea katika kijiji cha Nyakanazi unaoigharimu serikali shilingi bilioni mbili nukta sita.

Majaliwa amewaagiza viongozi wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimia vizuri miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ukiwemo na huo wa ujenzi wa kituo cha maegesho ya magari makubwa kwa maendeleo ya wananchi.

Pia, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo kuhakikisha eneo la Nyakanazi linapimwa na kuanisha matumizi ya kila eneo ikiwemo makazi, Huduma za Jamii, Viwanda, Viwanja vya Michezo na maeneo mbalimbali ya uwekezaji.

Kwa upande wake, Mhandisi wa TARURA wa wilaya ya Biharamulo, Julius Sumaye ambaye ndiye msimamizi wa ujenzi wa mradi huo amesema unalengo la kuongeza mapato ya halmashauri ili iweze kupunguza utegemezi kutoka Serikali Kuu.

Amesema halmashauri yao imetenga eneo la ukubwa wa hekta 10 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya uwekezaji ambapo kati yake hekta 3.2 zimetumika katika ujenzi kituo hicho, hekta 2.3 ni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi na hekta 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya biashara.

Mhandisi huyo amesema kwa awamu ya kwanza wameanza na ujenzi wa mradi wa kituo cha kuegeshea magari makubwa chenye uwezo wa kuegesha malori 300 kwa wakati mmoja. Mradi huo umefikia asilimia 48 ya utekelezaji wake.

 

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.