Star Tv

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo ameitaka Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuhakikisha watanzania wahitaji wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu wanawezeshwa.

Akizungumza katika Hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Sebastian Inoshi, wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) baina ya taasisi hizo leo Jijini Dodoma, Dkt. Akwilapo alisema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za Serikali kushirikiana katika kuwafikia wananchi na kutoa huduma.

Dkt. Akwilapo aliongeza kuwa ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa Watanzania wahitaji wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu wanapata mikopo ya elimu ya juu na kutimiza ndoto zao, hivyo upo umuhimu mkubwa wa TASAF na Bodi ya Mikopo kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kama inavyotarajiwa.

“Katika hili naomba niwape takwimu, mwaka 2019/2020, Serikali ilitoa TZS 450 Bilioni zilizowanufaisha jumla ya wanafunzi 132,392, Bajeti hii imeongezeka hadi kufikia TZS 570 Bilioni mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 ambazo zitawanufaisha jumla ya wanafunzi 160,000” -alisema Dkt. Akwilapo.

Aidha Dkt. Akwilapo ameitaka Bodi ya Mikopo na TASAF ziongeze kasi ya kuunganishwa kwa mifumo ya TEHAMA ili kuwezesha utambuzi wa haraka na uhakika wa wanafunzi wanaotoka katika kaya masikini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaopata udahili katika taasisi za elimu ya juu nchini na ambao wapo katika mpango wa TASAF wanapata mikopo ya elimu ya juu na kutimiza ndoto zao.

“Makubaliano haya yatasaidia kuongeza ufanisi katika kubadilishana taarifa, hivyo na HESLB imejipanga kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu, Wanafunzi wahitaji wahakikishe wanatimiza wajibu wao kwa kuomba mkopo kwa usahihi” - Alisema Badru.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga amesema taasisi hiyo itahakikisha inasimamia kwa umakini mkubwa malengo ya ushirikiano huo ili kuhakikisha wanafunzi wanaotoka katika kaya maskini wanapata mikopo ya elimu ya juu kutoka HESLB.

Ushirikiano huo unaiwezesha HESLB kama taasisi ya mikopo ya wanafunzi kupanga mikopo kwa wanafunzi wahitaji kutoka katika mpango unaoakiwa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.