Star Tv

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. Mafuzno hayo yamegusia  kuhusu Sheria zinazosimamia vyombo vya habari nchini Tanzania.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Ndugu Andrew Marawiti ambaye anasema mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo Wahariri na waandishi, katika vyombo vya habari kuhusu Sheria mbalimbali za uhudumu wa vyombo vya habari, (Media Act Service).

Huku upande mwingine ikiwa ni kuwajengea uwezo wahariri kuhusu mfumo wa sera za sheria za vyombo vya habari ili wasaidie kutumia nafasi zao kuleta mabadiliko kwa waandishi wa habari na jamii kwa manufaa ya taifa zima. Sheria hizo ni pamoja na EPOCA 2010, Sheria ya Takwimu, Sheria ya vyombo vya habari 2016, sheria ya kupata taarifa na Sheria ya mitandao. Huku akionyesha wajibu wa waandishi na wahariri wa Habari kuzifahamu vyema Sheria zinazosimamia taaluma ya Habari pamoja na Kanuni zake ambazo wataweza kutambua wajibu wao na majukumumu waliyonayo ili kuondokana na rapsha zinazojitokeza. Mafunzo haya yameendeshwa na wakufunzi tofauti akiwepo Jesse Kwayu na Jackiline Jones.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.