Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuongeza idadi ya Wizara, kuteua Mawaziri na Manaibu Waziri wapya na kuwahamisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri.

Katika mabadiliko hayo Rais Magufuli ameongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21, na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21.

Rais Magufuli ametangaza mabadiliko hayo Ikulu jijini Dar es Salaam akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

I. Waziri – George Mkuchika

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

I. Waziri - Selemani Jafo

II. Naibu Waziri - Joseph Kandege

III. Naibu Wazri – George Kakunda

Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

I. Waziri - January Makamba

II. Naibu Waziri - Kangi Lugola

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.

I. Waziri - Jenista Mhagama

II. Naibu Waziri - Anthony Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)

III. Naibu Waziri - Stella Ikupa (Walemavu)

Wizara ya Kilimo.

I. Waziri - Dkt. Charles Tizeba

II. Naibu Waziri - Dkt. Mary Mwanjelwa

Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

I. Waziri - Luhaga Mpina

II. Naibu Waziri - Abdallah Ulega

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

I. Waziri - Prof. Makame Mbarawa

II. Naibu Waziri - Mhandisi Atashasta Nditiye

III. Naibu Waziri - Elias Kwandikwa

Wizara ya Fedha na Mipango.

I. Waziri - Dkt. Philip Mpango

II. Naibu Waziri - Dkt. Ashatu Kijaji

Wizara ya Nishati.

I. Waziri - Dkt. Medard Kalemani

II. Naibu Waziri - Subira Mgalu

Wizara ya Madini.

I. Waziri - Angellah Kairuki

II. Naibu Waziri - Stanslaus Nyongo

Wizara ya Katiba na Sheria.

I. Waziri - Prof. Palamagamba Kabudi.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

I. Waziri - Dkt. Augustine Mahiga

II. Naibu Waziri - Dkt. Susan Kolimba

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).

I. Waziri - Dkt. Hussein Ali Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

I. Waziri - Mwigulu Nchemba

II. Naibu Waziri - Mhandisi Hamad Masauni

Wizara ya Maliasili na Utalii.

I. Waziri - Dkt. Hamisi Kigwangalla

II. Naibu Waziri - Josephat Hasunga

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

I. Waziri - William Lukuvi

II. Naibu Waziri - Angelina Mabula

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

I. Waziri - Charles Mwijage

II. Naibu Waziri - Mhandisi Stella Manyanya

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

I. Waziri - Prof. Joyce Ndalichako

II. Naibu Waziri - William Ole Nasha

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

I. Waziri - Ummy Mwalimu

II. Naibu Waziri - Dkt. Faustine Ndugulile Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

I. Waziri - Dkt. Harrison Mwakyembe

II. Naibu Waziri - Juliana Shonza

Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

I. Waziri - Mhandisi Isack Kamwelwe

II. Naibu Waziri - Jumaa Aweso

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bwana Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kabla ya Uteuzi huo Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri. Bwana Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dokta Thomas Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Wateule wote wataapisha Jumatatu tarehe 09 Oktoba, 2017 saa 3:30 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.