Aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama Cha Upinzani (CHADEMA) na kiongozi wa chama cha upinzani nchini Tanzania, Chadema,bwana Tundu Lissu ametunukiwa tuzo ya demokrasia.
Lissu ametunukiwa tuzo hiyo na Taasisi ya kimataifa ya 'International Democrat Union' kutokana na mapambano yake ya uhuru na demokrasia aliyoyafanya nchini Tanzania.
Mara baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba kutangazwa, Lissu alisema kuwa alikuwa akipokea vitisho vya kifo hatua iliomfanya kuondoka na kuelekea Ubelgiji.
Lissu alirejea Tanzania mwezi Julai mwaka huu ili kuwania nafasi ya urais ambapo alishindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28.