Star Tv

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kupandisha mishahara kwa watumishi iwapo atapewa ridhaa yakuwa rais kwa muhula wa pili.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akifanya mkutano katika uwanja wa TTC Korogwe mkoa wa Tanga wakati akinadi sera za chama hicho na kuomba ridhaa kwa wananchi kumchagua kuwa Rais na kuchagua wabunge na madiwani wa CCM.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, hiyo huku akisisitiza kuwa ili mipango mbalimbali iweze kufanikiwa ni lazima kujipanga kukusanya fedha na kutengeneza miundombinu.

“Maendeleo ni lazima yapangwe, bila kupangwa hakuna kitakachofanyika....Miaka mitano ilikuwa ya kujipanga ndio maana tulijenga vituo vya afya, zahanati, hospitali za mikoa”.-Dkt.Magufuli.

Mgombea Urais huyo amesema miaka mitano iliyopita, serikali imeweza kuajiri watumishi 74,000, pamoja na kuimarisha uchumi wa Tanzania.

Latest News

RAIS WA CHAD, IDRISS DEBY ATIMIZA MIAKA 30 MADARAKANI.
01 Dec 2020 14:48 - Grace Melleor

Desemba 1, 1990, Idriss Déby alichukua hatamu ya uongozi wa nchi ya Chad kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa, H [ ... ]

“HATUONDOKI CHADEMA, TUNAKATA RUFAA”- Halima Mdee.
01 Dec 2020 13:01 - Grace Melleor

Wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wa chama cha upinzani Chadema, wamesema wataendelea kuwa 'wanachama wa h [ ... ]

MTANZANIA ALIYETEKELEZA SHAMBULIZI CHUO CHA GARISSA AJINYONGA GEREZANI.
30 Nov 2020 10:05 - Grace Melleor

Mtanzania Rashid Charles Mberesero aliyehukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2019 baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.