Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt.Bashiru Ally ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili 10 ya wanafunzi waliofariki kwa kuungua na moto.
Ajali hiyo iliyotokana na moto ambao chanzo chake hakikujulikana mpaka sasa, uliteketeza bweni la watoto wa kiume katika shule ya msingi Byamungu Islamic iliyoko wilayani Kyerwa Mkoani Kagera na kupelekea watoto 10 kupoteza maisha papohapo.
Wanafunzi hao walifarika usiku wa kuamkia tarehe 14 Septemba, 2020, huku wanafunzi saba wakiwa wamejeruhiwa na mpaka sasa watano kati yao wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.
Jumla ya wanafunzi waliokuwepo kwenye bweni hilo wakati ajali hiyo ya moto inatokea ni 74.