Star Tv

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema Jerome Luanda ambaye ni msaidizi wa Bernard Membe yuko mikononi mwa polisi na anashangazwa na watu wanaosema ametekwa na watu wasiojulikana.

Kamanda Mambosasa amesema Luanda anashikiliwa na polisi kwa kosa la utakatishaji fedha.

“Na huyu nasema amekamatwa, anatuhumiwa kwa kosa la kutakatisha fedha, kwahiyo anayetaka kuthibitisha hilo ni suala la kuja tumueleze ukweli wa jambo hilo.”-Amesema Kamamnda Mambosasa.

Kauli hii ya Mambosasa imekuja baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa msaidizi huyo wa mgombea urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo alitekwa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.