Star Tv

Bingwa wa uzani mzito duniani Mike Tyson amezuiliwa kuhudhuria sherehe ya kupeana tuzo mjini Santiago, Chile.

Raia huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 51 ambaye aliwahi wakati mmoja kuhudumia kifungo jela kwa ubakaji, unyanyasaji na umiliki wa dawa za kulevya alirudishwa nyumbani na maafisa wa polisi wa idara ya uhamiaji.

Maafisa wa polisi katika uwanja wa Santiago walisema kuwa Tyson alirudishwa nyumbani kwa kufeli kuafikia sheria za uhamiaji.

Tyson alizuiliwa kuingia nchini Uingereza 2013 kutokana na matatizo yaliomkumba wakati wa nyuma.

''Baada ya kutathmini rekodi yake kulingana na sheria za uhamiaji ,wageni wote ambao walihukumiwa kwa kutekeleza uhalifu wowote hawaruhusiwi kuingia nchini humu'', polisi walisema.

Bingwa huyo mara mbili alihudumia miaka mitata jela katika kifungo cha miaka sita 1992 kwa kumbaka mgombea wa shindano la malkia wa urembo nchini humo.

Alikuwa bingwa wa uzani mzito mwenye umri mdogo katika historia ya uzani huo wakati alipomshinda Trevor Berbick 1986.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.