Star Tv

Papa Francis ameagiza marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya Vatican , kuanzia mwaka ujao.

Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu.

Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei .Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.

Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.

''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema.

''Ni kitu ambacho ni lazima kufutilia mbali licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa''.

Papa Francis ambaye pafu lake moja liliondolewa wakati alipokuwa kijana havuti sigara.

Wafanyikazi wa vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua pakiti tano za sigara kila mwezi kutoka kwa duka lisilotozwa ushuru.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.