Star Tv

Watu waliojihami kwa silaha wamewauwa wakulima 15 Kaskazini Magharibi mwa Jimbo la Katsina, katika kile, polisi wametaja ni kisa cha wizi wa mifugo.

Msemaji wa polisi Gambo Isah ameliambia shirika la AFP kuwa watu wapatao 200 waliojihami kwa bunduki walishambulia wakulima hao kwenye kijiji cha Yargamji na kuua watu 15, na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Nigeria ni moja ya nchi za Afrika Magharibi ambazo zinaendelea kukumbwa zaidi na utovu wa usalama kutokana na makundi mbalimbali yenye silaha, hasa makundi ya wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali, ikiwa ni pamoja na kundi la Boko Haram.

Mapema mwezi Juni watu wasiopungua hamsini waliuawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea katika vijiji viwili, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, mauaji ambayo yalidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State Afrika Magharibi (ISWAP).

Mashahidi wanasema watu waliojihami kwa silaha za kivita wakiwa katika magari walikabiliana na kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na serikali, lakini wanamgambo hao walizidiwa nguvu kutokana na idadi yao ndogo na hivyo kundi hasimu kutekeleza mauaji dhidi ya raia waliokuwa wakitoroka makazi yao, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.