Star Tv

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mpya, kuchukua nafasi ya Edouard Philippe, aliyejiuzulu na Baraza lake la Mawaziri baada ya chama tawala kufanya vibaya katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Uteuzi huo wa Castex, ambaye ni mwanasiasa wa Upinzani anayeegemea siasa za mrengo wa kati, umewashangaza wengi ambao hawakutarajia rais Macron angefanya uteuzi huo.

Castex kabla ya kuteuliwa katika nafasi hii ya juu nchini humo amekuwa akiongoza Kamati inayosimamia mapambano dhidi ya maambukizi ya Corona na kuoanekana kufanikiwa.

Baada ya uteuzi huu, anatarajiwa kutangaza baraza lake la Mawaziri huku rais Macron akiahidi kuwa serikali yake mpya sasa itakuwa na mwelekeo mpya wa kuhakikisha kuwa taofa hilo linaimarika tena baada ya janga la Corona.

Wachambuzi wa siasa nchini Ufaransa wanasema kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022, rais Macron ameanza maandalizi ya mapema kw aku,teau mwanasiasa wa upinzani kuwa Waziri Mkuu, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuchagliwa tena.

Aidha, wakati alipokuwa madarakani Edouard Philippe, alionekana kupata umaarufu mkubwa kumpita rais Macron, licha ya serikali yake kushuhudia maandamano makubwa mwaka uliopita ya vizibao vya njano ambayo yalikuwa yakipinga mageuzi ambayo walidai yanawapendelea matajiri.

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.