Jeshi la Korea Kaskazini limesema kwamba liko tayari kuingia katika eneo lisiloruhusiwa shughuli za kijeshi linalogawanya nchi hiyo na Korea Kusini ambapo Korea Kaskazini imetishia kutuma jeshi eneo salama la mpakani.
Tishio hilo linatokana na makundi yaliyoasi na kutorokea Korea Kusini yanayosambaza propaganda Korea Kaskazini.
Wikendi iliyoisha,Kim Yo-jong, dada wa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un, alisema kwamba ataagiza jeshi kuelekea eneo hilo.
Na sasa hivi jeshi linasema liko tayari kubadilisha eneo hil kuwa ngome yao na kugusia kuwa liko macho.
Wasiwasi kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiongezeka kwa muda sasa kwasababu ya vipeperushi ambavyo vimekuwa vikisambaa katika mpaka wa maeneo hayo mawili ambavyo kawaida huwa vinatumwa kwa njia ya maputo.
Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Jumanne amejibu vitisho hivyo kwa kusema kuwa inashirikiana na Marekani kufuatilia kwa karibu hatua za kijeshi upande wa Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini na Kusini zinagawanywa na eneo lisiloruhusiwa shughuli za kijeshi katika mpaka wake ambao umegawanya nchi hizo mbili tangu Vita ya Korea miaka ya 1950.
Jumanne, jeshi la Korea Kaskazini lilisema linafuatilia hatua inatakayochukuliwa na jeshi lake kwenda eneo hilo ambalo haliruhusiwi shughuli za kijeshi, huku Mkuu wa jeshi alisema liko katika hali ya tahadhari na tayari kutekeleza hatua yoyote itakayochukuliwa na serikali.