Star Tv

Maafisa wa afya Nchini China leo Mei 04,2020 Jumatatu wamebaini kuwa watu watatu wana maambukizi ya virusi vya Corona katika upande wa China Bara.

Licha kubaini uwepo wa watu hao walioambukizwa wametoa taarifa ya kutokuwa na kifo chochote kinachohusiana na ugonjwa huo ambacho.

Tume ya Kitaifa ya Afya nchini humo imesema kubainika kwa visa hivyo ni kwasababu wanafanya mikutano ya kila siku.

Maafisa hao wamesema watu wote watatu walioambukizwa virusi hivyo ni raia kutoka nchi za kigeni japokuwa hawajataja nchi hizo za kigeni ndio zipi.

Kwa jumla, kulingana na takwimu za tume hiyo, watu 82,880 wameambukizwa virusi vya Corona katika China Bara na kusababisha vifo vya watu 4,633. Huku takwimu zikionyesha kuwa zaidi ya watu milioni 3.5 wameambukizwa virusi vya Corona duniani.

China imeendelea kunyooshewa kidole cha lawama na Marekani kwamba ilipuuzia hatari ya ugonjwa wa Covid-19 na kusababisha nchi nyingi kuathirika na ugonjwa huo.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu na wataalam wa Afya wanaeleza kuwa dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambapo baada ya wiki moja au zaidi muathiriwa anaanza kukabiliwa na tatizo la kupumua.

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.