Star Tv

Ndege ya abiria ya Ufaransa iliyokuwa imewasili nchini Congo Brazaville kuwarudisha raia wa Ufaransa ,kurejea nyumbani kufutia janga la Corona,  imeshambuliwa kwa risasi na maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege wa Pointe-Noire.

Usimamizi wa safari za ndege nchini Congo-Brazzaville na Shirika la ndege la Ufaransa la Air France, zimesema tukio hilo halikukusudiwa na sasa ndege nyingine inasubiriwa kuwasafirisha raia hao wa Ufaransa.

Ndege hiyo iliwasili Jumamosi ili kuwarudisha nyumbani raia wa Ufaransa wanaoishi nchini Congo na kulingana na vyanzo kadhaa, tukio hilo lilitokea Jumamosi jioni kati ya saa 9:30 usiku. na 9:50 saa za Congo-Brazzaville.

Hata hivyo mamlaka ya uwanja wa ndege wa Pointe Noir imesema kuwa tukio hilo lilitokea kimakosa baada ya afisa kutoka kikosi cha walinzi wa mipaka kujichanganya mwenyewe na kufyatua risasi bila kukusudia.

Olivier Jallet ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege la Air France nchini Congo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amesema ndege hiyo ilishambuliwa kwa risasi mbili.

Ndege hiyo ilitarajiwa kusafirisha raia wa Ufaransa 110 Jumapili Aprili 12, baada ya kupata ruhsa maalumu kutokana na kuwa mipaka ya nchi ya Congo-Brazzavile inafungwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19.

Safari hiyo ilisogezwa mbele hadi leo Jumatatu na Balozi wa Ufaransa François Barateau alikutana Jumapili na wajumbe watatu wa serikali ya Congo akiwemo Jean-Claude Gakosso ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, ambaye katika barua alielezea masikitiko yake kwa serikali ya Ufaransa na kutangaza kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kujua sababu na kuwachukulia hatua kali wahusika.

Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wakati wa tukio hilo, Congo iliripoti kesi yake ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya Corona iliyoingizwa kutoka Ufaransa, mnamo Machi 14 na mpaka sasa watu 75 wamefariki dunia kwa Covid-19 nchini humo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.