Star Tv

Idadi ya waliokufa kwa virusi vya corona nchini Marekani kwa sasa ipo juu zaidi duniani baada ya kupita idadi ya nchini Italia.

Data za hivi karibuni kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonesha kwamba zaidi ya watu 20,000 nchini Marekani wamekufa kutokana na janga la corona.

Gavana wa New York Andrew Cuomo amesema Jumamosi kwamba vifo hivyo vinaendelea kudhibitiwa.

Ndani ya saa 24 alitangaza vifo vipya 783, na kusema kwamba siku kadhaa zilizopita jimbo hilo limeshuhudia idadi ya vifo karibu na hiyo.

Jimbo la New York limekuwa kitovu cha mlipuko wa virusi vya corona nchini Marekani, na kurekodi zaidi ya wagonjwa 180,000 kati ya wagonjwa 530,000 waliobainika nchini humo.

Kufikia Jumamosi, kila jimbo la Marekani lilikuwa limetangaza ugonjwa huo kama janga ikiwa ni hatua moja ya kukabiliana na mlipuko huo.

Zaidi ya watu 100,000 wamekufa na Covid-19 kote duniani tangu kuanza kwa virusi hivyo nchini China mwezi Desemba.

Kufikia Jumapili asubuhi, Italia ilikuwa imeripoti vifo 19,468 vya virusi vya corona huku Marekani ikiwa na vifo 20,608, kulingana na takwimu za hospitali ya Johns Hopkins.

Hadi kufikia sasa, wagonjwa 529,951 wa Covid-19 wameripotiwa kote nchini Marekani.

Daktari Anthony Fauci, mkuu wa magonjwa yanayoambukiza Marekani amesema, nchi hiyo imeanza kudhibiti na kushuhudia kupungua kwa visa na vifo vya ugonjwa wa corona lakini akasisitiza kwamba juhudi za kuuzuia kama vile kutokaribiana ziendelezwe.

Hatua za serikali zilizotolewa na Rais Donald Trump, kwa sasa bado zinaendelea kutekelezwa hadi Aprili, 30.

Rais anakumbana na shinikizo mara mbili, kukabiliana na mlipuko huo huku watu karibia milioni 16 wakipoteza ajira kwa sababu ya virusi hivyo katika wiki za hivi karibuni ilihali hatua zilizochukuliwa zinaendelea kudidimiza uchumi.

Katika taarifa yao walielezea hatua hiyo kama vitisho visivyo na msingi ambavyo vilikuwa kikwazo kwa uhifadhi wa pesa za kuokoa ajira.

                                    Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.