Mahakama ya Israel leo Machi 10, 2020 imekataa ombi la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu la kutaka kufungua kesi ya rushwa dhidi yake anbayo imeahirishwa hadi wiki ijayo.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Machi 17,2020 ambapo kwasasa imekuja wakati Netanyahu na washirika wake wa wakijaribu kuunda serikali huku wakikabiliwa na upinzani mkali kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.
Wabunge walioko upande wa Netanyahu ambaye ni Waziri Mkuu wa kwanza kushtakiwa akiwa madarakani, wameiambia mahakama hiyo ya wilaya mjini Jerusalem kwamba hawakupokea nyaraka zote za upande wa mwendesha mashtaka kuhusu kesi hiyo na wametaka wapewe muda wa siku 45.
Netanyahu anashtakiwa kwa tuhuma za udanganyifu, suala la rushwa na utumiaji mbaya wa madaraka pia akidaiwa kupokea zawadi kama takrima kinyume cha sheria ambapo kwa upande wake Waziri mkuu Netanyahu amekanusha madai hayo.
Mwisho.