Star Tv

Imeelezwa kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona nchini Italia imeongezeka kutoka 133 na kufikia 366 kwa siku moja.

Kwa mujibu wa shirika la kitaifa la utabiri na udhibiti wa matukio ya dharura wamesema maambukizi yatokanayo na virusi hivyo yameongezeka kwa asilimia 25% na kufikia 7,375 kutoka 5,883.

Ongezeko la maambukizi hayo limekuja wakati mamilioni ya watu wakichukua hatua zilizotangazwa siku ya Jumapili ili kudhibiti maambukizi.

Takribani watu milioni 26 mjini Lombardy na katika majimbo 14 chini ya sheria mpya ya karantini wameripotiwa kuhitaji ruhusa maalum ya kusafiri.

Waziri Mkuu Giuseppe Conte ametangaza kufungwa kwa shule, maeneo ya kufanya mazoezi, makumbusho, nyumba za starehe na maeneo mengine yanayokusanya watu wengi ambapo mazuio hayo yatadumu mpaka tarehe 3 mwezi Aprili.

Ongezeko hilo linamaanisha kuwa Italia kwa sasa ina idadi kubwa iliyothibitishwa nje ya China, ambapo tangu mlipuko wa corona ulipoanza mwezi Disemba huku taarifa zikieleza kuwa idadi hiyo imezidi Korea Kusini, ambayo ina idadi ya maambukizi 7,313.

Italia ni nchi mojawapo duniani yenye idadi kubwa ya watu wenye umri mkubwa ambayo wataalamu wa afya wamedhihirisha kuwa Virusi hivyo ni hatari hasa kwa wazee.

Miongoni mwa watu waliopata maambukizi hivi karibuni ni mkuu wa jeshi nchini humo Salvatore Farina ambaye baada ya kuhojiwa baadaye alisema alijisikia vizuri kwa alipofanya maamuzi ya kujitenga mwenyewe ili kuepuka kuambukiza wengine.

Aidha, mkuu wa Shirika la Afya duniani, WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameisifu Italia kwa kujitoa kwao kwa dhati kwa kuweka mazuio yanayokusanya watu wengi kwenye maeneo kama shule pamoja na makumbusho.

                   Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.