Star Tv

Jeshi la Israeli limesema limefanya mashambulio ya anga dhidi ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina mjini Gaza na Syria kujibu mashambulio yake ya roketi.

Jeshi hilo limesema limeyapiga maeneo ya Jihad kusini mwa mji mkuu wa Syria Damascus na katika ukanda wa Gaza siku ya Jumapili.

Katika hatua ya nadra ya Israeli kukubali mashambulio dhidi ya Syria, jeshi la Israeli lilisema kuwa lililenga " kitovu cha shughuli za kundi la jihadi la Kiislamu ".

Wakati Syria ikitoa taarifa kuwa majeshi yake ya ulinzi ya anga  yalifanikiwa kudungua makombora mengi ya Israeli, Watu wanne walijeruhiwa mjini Gaza, kulingana na taarifa kutoka maafisa wa afya, lakini hakuna ripoti za moja kwa moja juu ya vifo kutokana na mashambulio ya Israeli.

Mashambulio yaliyofanywa baada ya eneo la kusini mwa Israeli kupigwa na kundi la makombora takriban 20 ya roketi yaliyorushwa mapema jumapili  na hakuna ripoti juu ya majeruhi kwa upande wa Israeli

Uhasama huu ulianza Jumapili , wakati Israeli iliposema ilimuua mjumbe wa kikundi cha Jihad kwenye maeneo ya uzio wa mpaka na ukanda wa Gaza ambapo jeshi la Israeli limesema kuwa mwanaume huyo alikua akijaribu kuweka mtambo wa vilipuzi.

Ukanda wa video uliosambazwa sana kwenye mitandao ya habari ya kijamii ilionyesha tingatinga la Israeli likiuburuza mwili wa mwanaume huyo, jambo lililoibua ghadhabu miongoni mwa Wapalestina.

Baadhi ya Wapalestina walitoa wito wa ulipizaji kisasi na saa kadhaa baadae, maroketi yakafyatuliwa katika ukanda wa Gaza na ndipo uvamizi wa anga ukaanza.

Kundi la Jihad la kiislamu ambalo linaungwa mkono na Iran lilidai kuhusika na shambulio la maroketi, likiyataja kuwa ni jibu la mauaji ya mmoja wa wapiganaji wake aliyeuliwa kwenye eneo la mpaka wa Gaza.

Mapigano baina ya Israel na kundi la wanamgambo wa Jihad yalishamiri mwezi wa novemba, wakati mashambulio ya anga ya Israeli yalipomuua kamanda wa ngazi ya juu wa kikundi cha wanamgambo mjini Gaza.

Makabiliano baina ya vikosi vya Israeli na Wapalestina yalishuhudiwa mapema mwezi huu pia, siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza mpango wake wa amani, na kufungua ubalozi wa Marekani mjini Jerusalemu.

                                                             Mwisho.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.