Maafisa wa serikali ya China wamethibitisha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopoteza Maisha kutokana na homa inayosababishwa na virusi vya corona.
Mpaka sasa idadi ya watu waliokufa imefikia 425, wengi wa wahanga wakiwa katika mkoa wa Hubei, ilikoanzia.
Aidha, kulingana na maafisa wa serikali ya serikali ya China wamesema hadi sasa watu 20,438 katika maeneo yote nchini wameambukizwa homa ya virusi vya Corona katika.
Maafisa hao wameripoti pia visa 3,235, vingi vikiwa katika mkoa ulioathirika zaidi wa Habei ambapo kati ya watu 425 waliofariki kutokana na homa ya virusi hivyo hatari, 414 ambao wanatoka mkoa huo.
Viongozi wa China wamekiri kuwepo kwa mapungufu na changamoto katika juhudi za kuzuia kuenea zaidi kwa maradhi hayo.
Vyombo vya habari vya serikali nchini humo vimearifu kuwa hospitali mpya iliyojengwa kwa muda wa siku 10 tu imekamilika na imeanza kuwapokea wagonjwa.
Hospitali hiyo inavyo vitanda 1,000, na nyingine yenye vitanda 1,500 inatarajiwa kuwa tayari mnamo siku chache zijazo.
Mwisho.