Baraza la Senate la Marekani, linalodhibitiwa na Warepublican, limepinga jaribio la pili la chama cha Democratic kutaka nyaraka na ushahidi katika mchakato wa kumuondoa Rais Donald Trump madarakani.
Mchakato huo ambao ni watatu katika historia ya Marekani, ambapo maseneta wa Republican walipiga kura 53 dhidi ya 47 ya Wademocrat na kuzuia muswada kutoka kwa kiongozi wa Democratic Chuck Schumer, kutaka idara husika ya rekodi, iwasilishe ushahidi kuhusu shughuli za Trump na Ukraine.
Awali, baraza hilo lilipiga kura kwa njia hiyohiyo na kuzuia juhudi za Democratic kutaka nyaraka na rekodi kutoka ikulu ya Rais- White House kuhusiana na suala hilo.
Viongozi wa chama cha Democratic wamewashutumu wenzao wa Republic kwa kile ambacho wamekitaja kuwa udanganyifu katika mchakato huo.
Mwisho.