Star Tv

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC limerusha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.

Taarifa kutoka IRGC imesema kuwa, Iran imetoa jibu hilo kutokana na chokochoko za Marekani alfajiri ya leo, ambapo imelenga uwanja wa ndege wa kijeshi wa Marekani wa Ain al-Assad katika mkoa wa al-Anbar, magharibi mwa Iraq.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limeitaka Marekani iwaondoea wanajeshi wake wote katika nchi hiyo ya Kiarabu, likisisitiza kuwa halitatenganisha kati ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kujibu mapigo ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Soleimani.

Katika ujumbe wa IRGC wamesema; "Shetani mkubwa, yaani utawala wa kiistikbari wa Marekani utakabiliwa na vipigo vikali vya kuumiza, iwapo utachukua hatua nyingine ya kichokozi dhidi ya taifa kubwa la Iran."

Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imeongeza kuwa, pigo hilo dhidi ya Wamarekani wavamizi ni ushindi mkubwa kwa umma wa Kiislamu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif ameashiria jibu hilo la Iran katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika:

"Iran imechukua hatua madhubuti ya kujihami kwa mujibu wa Sura ya 51 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kulenga kambi ya jeshi ambayo ilitumiwa katika shambulizi la kioga dhidi ya raia na maafisa wetu wa ngazi za juu."

Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imethibitisha habari hizo za kuvurumishwa makumi ya makombora ya balestiki kuelekea katika kambi ya kistratajia ya jeshi la Marekani nchini Iraq.

Mapema jana, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema kisasi cha taifa la Iran kwa damu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha SEPAH kitakuwa kikali, madhubuti,cha kutisha na kamilifu.

                                                                                     Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.