Raia nchini Ufaransa na Ujerumani wanapiga kura leo katika siku ya mwisho ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya ambapo vyama vinavyopinga Umoja wa Ulaya pamoja na uhamiaji vinatumai kutoa changamoto kubwa.

Mbali ya Ujerumani na Ufaransa, ambayo ni mataifa yenye nguvu barani Ulaya, nchi nyingine karibu 20 wanachama wa Umoja huo zinapiga kura leo, ambayo ni siku ya mwisho ya uchaguzi huo wa Bunge la Ulaya. Zaidi ya wapiga kura milioni 400 wanashiriki uchaguzi huo katika mataifa 28 na matokeo rasmi yanatarajiwa baadaye leo jioni. Nchini Ujerumani, maoni ya umma ya kabla ya uchaguzi yalivipa nafasi ya ushindi wa asilimia 28 vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU na CSU. Wanasiasa kutoka vyama vikuu nchini Ujerumani walitumia siku za mwisho kabla ya uchaguzi kutoa onyo dhidi ya kukipigia kura chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, kinachopinga wahamiaji na Umoja wa Ualya.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW.

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.