Star Tv

Ni nia ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuwa mkutano kati yake na Rais wa Marekani Donald Trump uendelee, imeeleza taarifa ya vyombo vya habari vya Korea Kaskazini.

Hii ni kutokana na mkutano wa kushtukiza wa siku ya Jumamosi kati ya Kim na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in.

Rais Trump alisitisha mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni kuzungumzia mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini, lakini alisema Jumamosi kuwa mambo yanaendelea vizuri sana Wakati huo huo ujumbe wa Marekani uliripotiwa kwenda Korea Kaskazini siku ya Jumapili.

Balozi wa zamani wa Marekani nchini Korea Kusini, Sung Kim, atafanya mazungumzo na naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini kuhusu maandalizi ya mkutano, vyombo vya habari vya Marekani na Korea Kusini vimeeleza.

Mkutano huo ni matunda ya jitihada za kidiplomasia ambazo zilianza mwaka huu kujaribu kuondoa hali ya msuguano uliohofiwa kugeuka kuwa makabiliano ya kijeshi kati ya Korea Kaskazini, Korea Kusini, na Marekani.

Rais Moon amesema yeye na Rais Kim wamekubaliana mkutano wa tarehe 12 Juni uwe wa mafanikio na Kiongozi wa Korea Kaskazini kwa mara nyingine ameweka wazi nia yake ya kuondosha silaha za nuklia katika rasi ya Korea.

Lakini Moon amesema Kim hana uhakika kama nchi yake inaweza kuiamini Marekani na ahadi yake ya kumaliza mahusiano yao ya uhasama.

Viongozi hao wa juu watakuwa na mazungumzo zaidi siku ya Ijumaa.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.