Star Tv

Marekani itafungua ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa.

Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.

Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria.

Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina ambao wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mkuu wa badaye.

Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanwa.

Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa wastani wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.

Ni kipi kitafunguliwa na ni nani atahudhuria?

Ubalozi wa mdogo utaanza kutoa huduma kuanzia leo Jumatatu kwenye jengo la ofisi za ubalozi mjini Jerusalem.

Eneo lingine kubwa litatafutwa baadaye wakati ubalozi wote utahama kutoka mji wa Tel Aviv.

Sherehe za ufunguzi zilifanywa mapema ili ziweze kuenda sambamba na sherehe za miaka 70 za kuanzishwa taifa la Israel.

Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale ambaq watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.Kando na Ivanka Trump na Jared Kushner ambao wote ni washauri wakuu kwenye Ikulu ya White House, Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan watakuwa kwenye sherehe hiyo.

Muungano wa Ulaya umepinga vikali kuhamishwa kwa ubalzo huo na mabalozi wengine wa nchi za EU hawatahudhuria sherehe hiyo.

Hata hivyo wanadiplomasia kadhaa wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo waakilishi kutoka Hungary, Romania na Jamhuri ya Czech ambayo ilizuia taarifa ya pamoja ya EU kuhusu suala hilo.

Marais wa Guatemala na Paraguay pia nao wanatarajiwa kuhudhuria; nchi hizo zote mbili ziliamua kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem baada ya Trump kutoa tangazo hilo.

Israel na Palestina wanafanya nini?Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitoa wito kwa nchi zote kujiunga na Marekani na kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameutaja uamuzi wa Trump kama dafrao ya karne.Maefu ya Wapalestina wanakusanyika kuandamana kwenye ua unaotenganisha Israwl na ukanda wa Gaza.

Muda wa kuhamishwa ubalozi huo umezua wasi wasi wa kongezeka msukosko huko Gaza.

Tangu mwisho wa mwezi Machi zaidi ya wapalestina 40 wameuawa na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano ya mpakani. Mku wa shriika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ameilaumu Isreal kwa kutumia nguvu nyingi.

Hali ya mji wa Jerusalem ndiyo chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina.

Tangu mwaka 1967 Israel ilijenga makao mengine kwa karibu wayahudi 200,000 huko Jerusalem mashariki.

Makao hayo yanatajwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa, licha ya Israel kupinga hilo.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.