Star Tv
Wanakijiji wanasema kuwa utamaduni huu ambao ulianza enzi za utumwa wakati mababu zao walipozuiwa kusherehekea Krismasi tarehe 24 Desemba kama ilivyo kawaida kwa madhehebu mengi ya Kikristo. Badala yake waliamua kuchagua katikati mwa mwezi wa Februari na utamaduni huu umeendelea tangu wakati huo. Fataki, muziki na densi huwa sehemu ya sherehe hizo za kuvutia. "Watu waliotufanya watumwa walisherehekea Krismas Desemba na hatukuruhusiwa kuwa na mapumziko siku hiyo, lakini tukaambiwa tuchague siku nyingine," alisema, Holmes Larrahondo, mratibu wa sherehe. "Katika jamii yetu tunaamini kwamba mwanamke anapaswa kufunga siku 45 baada ya kujifungua, kwa hivyo tunasherehekea Krismas sio mwezi Disemba, bali Februari, kwa hiyo Maria anaweza kudensi pamoja nasi," aliongeza Bw Larrahondo. Wakati wa kuabudu, sherehe hizo huitwa "sherehe za kutoa heshma kwa Mungu wetu kwa namna yetu." Kama sehemu ya sherehe hizi, wanakijiji hutembelea nyumba mbali mbali "wakimtafuta mtoto Yesu", ambaye huwakilishwa na sanamu ya mbao ambayo hutunzwa na mmoja wa wanavijiji katika nyumbani kwake kwa kwa kipindi cha mwaka kilichosalia. Pale sanamu inapopatikana, hutembezwa kijijini na wakazi wa rika zote waliovalia kama malaika na wanajeshi. Wacheza densi, hucheza densi inayoitwa fuga; ambapo hucheza wakiigiza hatua za watumwa waliofungwa minyororo. Sherehe humalizika majira ya asubuhi mapema.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.