Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza janga hilo kuwa limekwisha nchini humo, Ambapo amebainisha kuwa "hata kama idadi ya Wamarekani ambao wamekufa kutokana na Covid inaendelea kuongezeka lakini janga hilo halipo nchini, ingawa bado tuna tatizo ila hali inaimarika kwa kasi".

Katika mahojiano na kipindi cha CBS cha 60 Minutes kilichopeperushwa Jumapili, Biden alisema kuwa Marekani bado inafanya "kazi nyingi" kudhibiti virusi. Ukigundua, hakuna mtu aliyevaa barakoa, "Kila mtu anaonekana kuwa katika hali nzuri ... Nadhani inabadilika."

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alisema wiki iliyopita kwamba mwisho wa janga hilo unaonekana, huku  Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya Wamarekani 400 kwa wastani wanafariki kutokana na virusi kila siku.

Lakini maafisa wa utawala waliambia vyombo vya habari vya Marekani Jumatatu kwamba maoni hayo hayaashiria mabadiliko ya sera na hakukuwa na mipango ya kuondoa dharura inayoendelea ya afya ya umma ya Covid-19.

Mnamo Agosti, maafisa wa Wamerekani waliongeza dharura ya afya ya umma, ambayo imekuwa tangu Januari 2020, hadi 13 Oktoba.

Aidha takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonyesha kuwa wastani wa siku saba wa vifo kwa sasa unasimama zaidi ya 400, na zaidi ya 3,000 wamekufa katika wiki iliyopita.

Maafisa wa afya ya umma wameelezea matumaini ya tahadhari katika wiki za hivi karibuni kwamba ulimwengu unaelekea kupona kwa janga, lakini wanaendelea kuwasihi watu kuwa waangalifu.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.