Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden amesema wafuasi wa ajenda ya Donald Trump ya "Make America Great Again" (Maga) ni tishio kwa demokrasia.

Rais Biden ametoa tamko hilo katika hotuba yake ya kwanza huko Pennsylvania ambapo amesema Viguvugu la Maga limedhamiria kurudisha nchi hiyo nyuma. 

Hotuba hiyo inakuja miezi miwili kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula, ambao utaamua usawa wa madaraka huko Washington.

Rais wa chama cha Democratic ametoa hotuba yake Alhamisi usiku kutoka Ukumbi wa Uhuru huko Philadelphia, ambapo Azimio la Uhuru wa Marekani lilitiwa saini.

Akitumia mada yake ya kampeni ya 2020 kuwatia "moyo Wamarekani". Alisema hakuwa akiwashutumu Wamarekani wote milioni 74 waliompigia kura Trump miaka miwili iliyopita.

"Sio kila Republican, ama Warepublican wengi, ni Maga Republican, lakini hakuna swali kwamba chama cha Republican leo kinaongozwa, kinaendeshwa na kutishwa na Donald Trump na Maga Republican, na hiyo ni tishio kwa nchi hii."

Aidha Rais Biden amesema wafuasi wa Trump walichukulia umati wa watu ambao walivamia Bunge la Marekani mwaka jana kama wazalendo badala ya waasi.

"Kwa muda mrefu tulijiambia kwamba demokrasia ya Marekani imehakikishwa. Lakini sivyo. Tunapaswa kuitetea. Ilinde. Simameni kwa ajili hiyo. Kila mmoja wetu."

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.