Kanali wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Tehran.
Watu wawili ambao hawakujulikana wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki wanaripotiwa kumpiga risasi Kanali Sayad Khodai mara tano kwenye gari nje ya nyumba yake.
Kufikia sasa, hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi la Jumapili, na msako unaendelea kuwatafuta watu hao wenye silaha.
Kanali Khodai alikuwa mwanachama mkuu wa Kikosi cha wasomi cha Quds, tawi la IRGC ambao wanaendesha operesheni nje ya taifa hilo.
#ChanzoBBC