Ukraine imethibitisha kwamba mamia ya wapiganaji wake waliokuwa wamekwama kwa zaidi ya miezi miwili katika mji wa Mauripol wameokolewa.
Naibu waziri wa ulinzi Hanna Maliar amesema kuwa wanajeshi walioumia vibaya 53 walipelekwa katika mji wa Novoazovsk, unaoshikiliwa na Urusi.
Hanna amesema kuwa wengine 211 walikombolewa kwa kutumia njia za kibinadamu kuelekea Olenivka mji mwingine unaodhibitiwa na waasi.
Awali Urusi ilisema mkataba umefikiwa wa kuwakomboa wanajeshi waliojeruhiwa.
Shirika la Habari la Reuters limeripoti kwamba takriban basi kumi na mbili zilizowabeba wapiganaji wa Ukraine waliokuwa wamekwama katika kiwanda kilichozingirwa zilionekana zikiondoka kusini mwa mji huo wa bandari jana Jumatatu jioni.
#ChanzoReuters
#ChanzoBBC