Mazoezi makubwa zaidi katika historia ya Baltics ya Muungano wa kijeshi wa NATO yanatarajiwa kuanza baadaye hii leo.
Mzoezi hayo yatafanyika katika taifa la Estonia kwa kipindi cha wiki mbili na yatawahusisha wanajeshi 15,000 kutoka nchi kumi, zikiwemo Uingereza, Marekani na wajumbe wa hivi karibuni wa Muungano wa NATO ambao ni Finland na Sweden.
Licha ya kwamba mazoezi hayo huwa yana lengo la kukabili maadui katika mataifa ya Baltic na yalikuwa yamepangwa hata kabla ya Urusi kuanza uvamizi nchini Ukraine, mazoezi haya sasa yameibua kwa kiasi kikubwa wasiwasi baina ya NATO na Urusi.