Star Tv

Bei ya mafuta imeelezwa kupanda hadi kiwango cha juu zaidi tangu 2008 baada ya Marekani kusema kuwa inajadili vikwazo vinavyowezekana kwa bidhaa za Urusi na washirika wake.
Brent crude - alama ya kimataifa ya mafuta - ilipanda hadi zaidi ya $139 kwa pipa, kabla ya kurudi chini hadi $130.

Masoko ya nishati yametikiswa katika siku za hivi karibuni kutokana na hofu ya usambazaji iliyosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Wateja tayari wanahisi athari ya gharama ya juu ya nishati kadiri bei ya mafuta na bili za za majumbani zinavyoongezeka.

Masoko ya hisa barani Asia yalishuka siku ya Jumatatu, huku kampuni za Nikkei za Japan na Hang Seng huko Hong Kong zikishuka kwa zaidi ya 3%.

Siku ya Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema utawala wa Biden na washirika wake wanajadili vikwazo vya usambazaji wa mafuta ya Urusi.
Wachambuzi wanabainisha kuwa vikwazo vya mafuta vya Urusi vitakuwa ongezeko kubwa katika kukabiliana na uvamizi wa Ukraine na kunaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa dunia.

#ChanzoBBC

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.