Maafisa katika mji wa Argentina wa Buenos Aires, wamejaribu kuzuia mauzo ya mihadarati aina ya 'Cocaine' baada ya kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 70 kulazwa hospitalini baada ya kutumia dawa hiyo ya kulevya.
Maafisa wamewaonya wavutaji ambao hivi karibuni walinunua 'cocaine' kuacha kuitumia mara moja.
Akielezea kuhusu kisa hicho, mwandishi wa habari aliyeko Buenos Aires - Frankie Deges, amesema: "Tetesi mbali mbali zinazunguka kuhusu ni nini hasa kilichotokea, ikisemekana kuwa dawa hiyo ilichanganywa na sumu ya kuua panya".
Polisi tayari wamewakamata watu 10 wakiwashuku kuchanganya 'cocaine' na madawa.