Star Tv

Polisi wa Uholanzi wanasema wamempata mtu akiwa hai katika sehemu ya gurudumu la ndege iliyotua katika uwanja wa ndege wa Amsterdam wa Schiphol kutoka Afrika Kusini.

Safari za ndege kutoka Johannesburg hadi Amsterdam huchukua takriban saa 11, huku ndege ya mizigo ikiaminika kusimama mara moja, jijini Nairobi, Kenya.

Mwanaume huyo alipatikana akiwa hai katika sehemu ya gurudumu upande wa pua ya ndege na alipelekwa hospitalini akiwa katika hali nzuri," msemaji wa Polisi wa Kijeshi wa Uholanzi Joanna Helmonds aliambia shirika la habari la AFP.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa Uholanzi NOS, joto la mwili wa mtu huyo liliongezeka katika eneo la tukio na wakati gari la wagonjwa lilifika, aliweza kujibu maswali ya msingi.

Kulingana na data ya ndege, ndege pekee ya Cargolux ya mizigo kutoka Johannesburg hadi Schiphol Jumapili pia ilisimama Nairobi na haijajulikana bado iwapo mwanaume huyo alipanda ndege hiyo nchini Afrika Kusini au Kenya.

#ChanzoBBC.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.