Mahakama nchini Myanmar imemhukumu kiongozi aliyeondolewa madarakani Aung San Suu Kyi kifungo cha miaka minne zaidi, katika mfululizo wa kesi za hivi karibuni alizopatikana nazo.
Bi su Kyi alitiwa hatiani kwa kumiliki kwa njia haramu na kuagiza vifaa vya mawasiliano vya ‘walkie-talkie’ na kuvunja sheria za Covid-19.
Bi Suu Kyi pi alipatikana na hatia kwa mara ya kwanza mwezi Desemba, na kupunguziwa kifungo cha miaka miwili jela.
Amewekwa kizuizini tangu mapinduzi ya kijeshi mwezi Februari mwaka jana na anakabiliwa na mashtaka kadhaa, ambayo yote anayakanusha.Wamelaaniwa sana kuwa ni wadhalimu.
Inaaminika kuwa mashtaka ya Jumatatu yalitokana na wakati wanajeshi walipopekua nyumba yake siku ya mapinduzi na vikosi vinavyoongozwa na Jenerali Min Aung Hlaing, waliposema waligundua vifaa hivyo.