Kampuni kubwa ya dawa nchini Marekani inatafuta idhini ya haraka ya kuweza kutibu virusi vya corona kwa watu wazima.
Merck imesema dawa ya molnupiravir, ambayo ni vidonge inawalenga wagonjwa ambao wako kwenye hatari ya maambukizi na ambao wamelazwa hospitalini .
Kampuni hiyo inatafuta idhini kutoka Mamlaka ya dawa na chakula nchini Marekani ili kuruhusu matumizi ya dawa hizo.
Merck inafanya kazi na Ridgeback Biotherapeutics na tayari imeshauza imeuza dozi 1.7m ya tiba kwa serikali ya Marekani.