Star Tv

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameamuru kuondolewa kwa marufuku dhidi ya mtandao wa kijamii wa Twitter, ikiwa kampuni hiyo ya kubwa ya teknolojia itafikia masharti Fulani yanayotakiwa.

Rais Buhari alisema Wanigeria wanaweza kuendelea kutumia mtandao huo kwa ajili ya "biashara na masuala mengine muhimu".

Katika hotuba yake ya kuadhimisha sikukuu ya uhuru wa nchi hiyo, Rais alisema kwamba kamati maalum ya ofisi yake inajadiliana na Twitter kuhusu masuala kadhaa ya usalama wa kitaifa, ushuru wa haki na utatuzi wa mizozo.

Serikali ya Nigeria ilipiga marufuku huduma zaTwitter tangu mwezi Juni baada ya mtandao huo wa kijamii kufuta ujumbe tata wa Rais Buhari.

Marufuku hiyo ilikosolowe vikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanaharakati wa kutetea uhuru wa vyombo vya habari.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.