Karibu theluthi mbili ya wapiga kura wa Uswizi wameunga mkono ndoa ya jinsia moja katika kura ya maoni.
Asilimia 64 waliunga mkono hatua hiyo, na kuifanya kuwa moja ya nchi za mwisho magharibi mwa Ulaya kuhalalisha ndoa za jinsia moja.
Wanaharakati wamepongeza kura hiyo kama hatua ya kihistoria kufikia haki za wapenzi wa jinsia nchini humo.
Kabla ya kura hiyo, makundi ya kidini na vyama vya kihafidhina vilipinga mpango huo vikisema unahujumu maadili ya familia.
Uswisi imeruhusu wenza wa jinsia moja kusajili uhusiano wao tangu 2007, lakini haki zingine zimedhibitiwa.
Hatua hiyo itawawezesha wapenzi wa jinsia moja kusaili watoto.
Inafanya Uswizi kuwa nchi ya 30 duniani kuhalalisha ndoa ya wapenzi wa jinsia moja.
Hatua hiyo itawawezesha wapenzi wa jinsia moja kusaili watoto na inafanya Uswizi kuwa nchi ya 30 duniani kuhalalisha ndoa ya wapenzi wa jinsia moja.
Waziri wa Haki Karin Keller-Sutter amesema ndoa ya kwanza ya jinsia moja itafanyika mwezi Julai mwaka ujao.
#ChanzoBBCSwahili