Star Tv

Mamlaka ya Afghanistan imethibitisha kwamba mwanasoka kijana alifariki dunia baada ya kujaribu kuondoka nchini humo kwa kudandia ndege ya jeshi la Marekani na kuanguka uwanja wa ndege wa Kabul.

Zaki Anwari, 19, alikuwa ameichezea timu ya taifa ya vijana ya Afghanistan, Pia maelezo zaidi ya ni lini alifariki dunia bado hayajawekwa wazi.

Tangu Taliban kuteka nchi ya Afghanistan, maelfu ya watu wamejitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, wakati ambapo nchi za Magharibi zinakimbilia kuhamisha raia wao kutoka Afghanistan.

Picha ziliibuka Jumatatu zikionyesha mamia ya watu wakikimbia kufuata ndege ya jeshi la anga la Marekani wakati ikishuka kwenye barabara ya kupaa, Ambapo watu wengine walionekana wakishikilia upande mmoja wa ndege.

Ripoti za vyombo vya habari vya eneo zinasema kwamba watu wasiopungua wawili waliuawa baada ya ndege hiyo wakati ikiwa inapaa.

Kikosi cha anga cha Marekani pia kimethibitisha kuwa mabaki ya binadamu yalipatikana katika vifaa vya kutua vya ndege baada ya kuwasili Qatar.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.